Now you can stream your call to millions via YouTube Live

Je, umetulia nyumbani?

Kwa njia iliyosalama jiunge na mjadala kwa njia ya maandishi, sauti au video. Tuko nawe ili kuhakikisha kuwa mawazo na hoja zako zimewasilishwa vikamilifu na kwa njia iliyosalama bila kuhatarisha taarifa kukuhusu

Je, umetulia nyumbani?

Kwa njia iliyosalama jiunge na mjadala kwa njia ya maandishi, sauti au video. Tuko nawe ili kuhakikisha kuwa mawazo na hoja zako zimewasilishwa vikamilifu na kwa njia iliyosalama bila kuhatarisha taarifa kukuhusu

Vipengele vya Gumzo

Hakuna kupimiwa hata kamwe, muda wa mazungumzo. Wasiliana na wenzako kwa muda uupendao, na hakikisha ujumbe wako umefika.

Video na Sauti

Mitandao yetu ya mawasiliano yanakupa uhuru wa kuchagua jinsi unavyotaka kuwasiliana. Tuna vyumba vya mawasiliano vinavoyo tumia njia ya maandishi pekee na ni bure, haulipii chochote. Kama wataka kuchangamsha maathiriano yako, chagua vyumba vya mawasiliano vinavyotumia sauti ama video angavu.

Mitambo Salama

Tumetekeleza sera madhubuti na kuwaweka wasimamizi kuhakikisha mitambo yetu ya mawasiliano ina kupa mahali salama pa kufanya mikutano na kuzungumza na wenzako. Tunavyo vituo vya wanawake pekee, vituo vya kibinafsi, na vituo vyenye mada kuhakikisha uko salama na unajivinjari.

Mwenyeji Afrika

Seva zetu zimehodhiwa hapa Afrika, ili kuifaidi Afrika. Hii inawezesha mawasiliano mwafaka na unauhakika kwamba maongezi yako hayapitishwi kwenye seva zilizoko Silicon Valley ama Uchina. Mitandao yetu ni ya kisasa na ya hali ya juu kuhakikisha signali yako haisafirishwi mbali.

Faragha ya Mawasiliano

Mifumo yetu ya mawasiliano ni dhabiti kuhakikisha faragha ya mawasiliano yako. Tunayo mifumo madhubuti inayohakikisha usalama na faragha ya mawasiliano yako. Mitambo yetu imesimbwa vilivyo kutumia teknolojia ya usalama wa mawasiliano. Kabla ya kujisajili, tunahitaji uthibitisho mwingi wa mtumiaji kuliko washindani wetu; mpango huu unatuwezesha kukulinda wewe.
Mawasiliano yote (maandishi, sauti au video) kati yako na seva yamesimbwa na yanapitishwa kupitia https na media imesimbwa kwa kutumia teknolojia ya WebRTC.

Mawasiliano kati ya watu wawili hapa Gumzo yamasimbwa kwa njia ya P2P.

Rahisi kujiunga

Hauhitaji kupakua chochote kutoka kwenye mtandao ili uweze kutumia Gumzo. Kujisajili ni rahisi na haraka sana kwa kutumia uthibitisho wa SMS.

Ushirikiano wa skrini

Ushirikiano wa skrini ukitumia Gumzo ni rahisi; inaruhusu timu yako kutatua maswala mbali mbali kwa haraka, kubadilishana mawazo na maoni, na pia kuwasiliana na wateja wako.

Upambaji wa chumba

Una uhuru wa kurembesha chumba chako cha mawasiliano kwa kutumia rangi na nembo unazozipenda ama zinazokuwakilisha wewe ama biashara yako.

Viungo rahisi vya chumba

Rahisi kukumbuka – rahisi kujiunga.

Jisajili ili kuanza kutumia

Utahitaji nambari yako ya simu tu ili kujisajili.
Tunakuahidi hatutawahi peana ama kuuza data yako kwa mtu yeyote ama kukutumia barua taka.
Skip to content