Now you can stream your call to millions via YouTube Live

ASILI YETU

Jua mengi kutuhusu

Asili Yetu

Usiku Games ni kampuni ya ICT kutoka Kenya iliyoanzishwa ili kupambana na janga la kamari kwa vijana barani Afrika. Lakini tulipokumbwa na janga kubwa la virusi vya korona, tuligundua kuwa jukwaa letu la mawasiliano tulilolitumia katika michezo yetu, linaweza kusaidia kuleta familia pamoja, na kuwezesha uchumi wetu kuendelea kuimalika kwa kuwapa wanabiashara wa hapa Afrika na watu binafsi jukwaa la kuwasiliana ambalo wanaweza kulitegemea, ambalo ni salama na lenye bei nafuu. Miezi miwili baadae, Gumzo ikaanzishwa, jukwaa la kwanza na la kipekee la mikutano ya video ambalo limetengenezewa barani Afrika kuifaidi Afrika.

Gumzo ni Salama

Mawasiliano yote katika Gumzo yamesimbwa, kuhakikisha mazungumzo yako ni faragha na yako salama. Kama mazungumzo ni kati ya watu chini ya wanne, siginali itasimbwa mwisho hadi mwisho. Kwa mazungumzo ama mkutano kati ya watu wengi, siginali inasimbwa kati ya kila mtu na seva kuu. Iwapo unahitaji mkutano wenye usalama zaidi, tunaweza hodhi mkutano huo kwenye seva zilizoko kwenye vituo vyenyu vya data.

Imetengenezewa Kenya, Kuwafaidi Wakenya

Tunajivunia kuwa Gumzo imetengenezewa hapa Kenya na Usiku Games, kampuni ya ICT. kila mawasiliano unayotekeleza kwa kutumia Gumzo inasaidia kuunda ajira na kusaidia na pia kuimarisha uchumi hapa Kenya. Malipo yote yanayotolewa yanabaki hapa Kenya. Wakati huu wa janga la COVID-19, tunatoa 50% ya malipo yote ya Gumzo kugharamia mipango ya kupambana na Corona nchini.

Jisajili ili kuanza kutumia

Utahitaji nambari yako ya simu tu ili kujisajili.
Tunakuahidi hatutawahi peana ama kuuza data yako kwa mtu yeyote ama kukutumia barua taka.
Skip to content