Now you can stream your call to millions via YouTube Live

Jinsi tulivyo wa kipekee

Gumzo inajivunia kutengenezewa hapa Kenya na Usiku Games; kampuni ya ICT. mawasiliano yote unayoyafanya kwa kutumia Gumzo yanaunda ajira hapa na kuimarisha uchumi hapa Kenya. Ada yote yanayotokana na matumizi ya Gumzo yanabaki hapa Kenya. Kwa wakati huu wa janga la COVID-19, Gumzo inatoa 50% ya ada kufadhili mipango ya kupamabana na virusi vya Corona hapa Kenya.

Gumzo ni rahisi kuitumia

Gumzo ni tofauti na majukwaa mengine. Hauhitaji kupakuwa programu ama viongezi ili kusanidi. Mawasiliano yote ya Gumzo hufanywan kwenye kivinjari, hii inaiwezesha kutumika kwenye simu mahiri na kompyuta. Punde unapojisajili na kupata na akaunti iliyodhibitishwa, unaweza kujiunga na mkutano kwa mbofyo mmoja.

Gumzo ni salama

Mawasiliano yote kwenye Gumzo yamesimbwa kuhakikisha mazungumzo yako in ya faragha na ni salama. Kama mazungumzo ni kati ya watu chini ya wanne, siginali itasimbwa mwisho hadi mwisho. Kwa mazungumzo ama mkutano kati ya watu wengi, siginali inasimbwa kati ya kila mtu na seva kuu. Iwapo unahitaji mkutano wenye usalama zaidi, tunaweza hodhi mkutano huo kwenye seva zilizoko kwenye vituo vyenyu vya data.

Gumzo kwenye Biashara

Gumzo inazo zana za kitaalamu ambazo unahitaji kufanya mikutano ya video. Gumzo imejumuisha zana kama mfumo kamili wa uwasilishaji, ushirikiano wa skrini na njia rahisi ya kupata maoni kutoka kwa waliohudhuria. Kwa wakati huu, tunaongeza vipengele vitakavyo kuwezesha kurekodi mawasiliano na kunakili maandishi ya mkutano. Vipengele hivi vitakuwezesha kusambaza na kuhifadhi kumbukumbu za mkutano wako.

Gumzo kwenye Burudani

Kando na kufanya mikutano ya kibiashara, unaweza jumuika na kuwasiliana na ndugu na marafiki wako kwenye Gumzo. Tumejumuisha vipengele kadhaa vya kufurahisha vinayoifanya Gumzo kuwa ya kipekee, na kusaidia kupunguza makali ya uchovu na kutengana haswaa wakati huu kuna vikwazo vya kusafiri. Unapotumia Gumzo, unaweza kucheza michezo na kutazama sinema pamoja na wenzako, hivi kama mpo pamoja.

Jisajili ili kuanza kutumia

Utahitaji nambari yako ya simu tu ili kujisajili.
Tunakuahidi hatutawahi peana ama kuuza data yako kwa mtu yeyote ama kukutumia barua taka.
Skip to content