MASWALI YA ULIZWAYO
Tuna majibu
Je, nawezaje kuanzisha mawasiliano ama kuhudhuria mkutano kwa Gumzo?
Kujiunga na chumba cha mazungumzo, utahitaji kiunga cha chumba hicho (URL). Kiunga hicho unaweza kukipata kutoka kwa mwenyeji wa chumba cha mazungumzo. Kabla haujajiunga na mazungumzo, utahitajika kuhisajili kwa kutumia uthibitisho wa SMS na kutengeneza wasifu wako, yaani jina lako rasmi, picha ya wasifu na jina la kutumia.
Je, nawezaje kutengeneza akaunti ya Gumzo?
Ili kutengeneza akaunti ya Gumzo, utahitaji nambari ya simu iliyosajiliwa. Baada ya kuingiza nambari yako ya simu, utapata ujumbe mfupi ambao utakuwezesha kuthibitisha akaunti yako na utaweza kujaza maelezo ya wasifu wako, yaani jina lako rasmi, picha ya wasifu na jina la kutumia. Baada ya kujisajili kikamilifu, utaweza kutengeneza vyumba vya mawasiliano kwa malipo yanayo anzia KES 100.
Je, nawezaje kuwaalika wenzangu?
Ili kuwaalika wenzako kwenye chumba chako cha mawasiliano, utahitajika kuwapa kiunga (URL) cha chumba chako. Kisha, wenzako watahitajika kujisajili kwa kutumia nambari zao za simu alafu utapata arifu wakiwa tayari kujumuika nawe.
Je, Gumzo ni bure?
Naam, Gumzo ni bure kwa wanao hudhuria mikutano lakini kuwa mwenyeji wa mkutano, utahitaji kulipa KES 100. Kwa maelezo zaidi kuhusu malipo yetu, bonyeza hapa
Utangamano wa Gumzo
Gumzo inatumia kivinjari pekee, hii inaiwezesha kufanya kazi safi kwa mahitaji kidogo. Lakini, ili uweze kufurahia uzoefu mzuri, kompyuta yako lazima ikidhi viwango hivi vya chini;
- Lazima iwe na kivijari cha kisasa na kinachotambulika kama vile Chrome, Safari ama Firefox
- Lazima iwe na mfumo endeshi wa kisasa kama vile MacOS Mojave ama Windows 10.
- Lazima iwe a na muunganisho thabiti wa mtandao wa intaneti.
Jisajili ili kuanza kutumia
Utahitaji nambari yako ya simu tu ili kujisajili.
Tunakuahidi hatutawahi peana ama kuuza data yako kwa mtu yeyote ama kukutumia barua taka.